JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OSWE BOYS SECONDARY SCHOOL P.O. BOX 665 MBOZI – SONGWE EMAIL: osweboys@gmail.com WEBSITE:www.osweschools.ac.tz |
TEL: 0752- 398224 HEAD OF SCHOOL : 0742 - 697782 VICE HEAD OF SCHOOL : 0764 -961755 ACADEMIC |
Kwa mzazi/ mlezi wa
………………………………………………………………
YAH: MAELEZO YA AWALI KWA MWANAFUNZI ANAYEJIUNGA NA
SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA OSWE.
A: UTANGULIZI
Uongozi wa shule ya sekondari ya wavulana oswe, unayo furaha kukujulisha kuwa mtoto wako amechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2025 katika shule hii.
Shule hii ni ya BWENI TU na ni shule ya wavulana tu. Masomo yanayofundishwa katika shule hii ni kama ifuatavyo; ENGLISH, LITERATURE IN ENGLISH, BASIC MATHEMATICS, BIOLOGY, PHYSICS, CHEMISTRY, CIVICS, HISTORY, GEOGRAPHY, KISWAHILI, INFORMATION AND COMPUTERS STUDIES.
Pamoja na kwamba baadhi ya vitabu vya masomo hayo vipo hapa shuleni, mwanafunzi anashauriwa kuja na vitabu vyake vya ziada vitakavyomsaidia katika masomo yake. Mhula wamasomo utaanza tarehe 7/01/2025 siku ya Jumapili hivyo mwanafunzi anatakiwa kuripoti kuanzia saa 2.00 asubuhi lakini isiwe baada ya saa11.00 jioni. Masomo yataanza rasmi tarehe 8/01/2024 asubuhi siku ya jumatatu.
B. SHULE ILIPO
Shule ipo mkoani SONGWE, wilaya ya MBOZI katika kijiji cha CHIMBUYA. Ipo pembezoni mwa barabara kuu MBEYA hadi TUNDUMA. Shule iko upande wa kusini mwa kituo cha mabasi cha CHIMBUYA YA KWANZA kutoka MBEYA na CHIMBUYA YA PILI kutoka tunduma. Kuna umbali wa½ km kufika shuleni.
Kwa wanafunzi wanaotoka mikoa ya Dar es salaam,Morogoro, n.k wanashauriwa kutumia usafiri wa mabasi ya ABC ,NEW FORCE, ABOOD NA DODOMA ABC AU NGASERE AU SHABIBY au mabasi yoyote yanayoishia TUNDUMA yatawafikisha salama. Kwa mabasi makubwa unateremka kituo cha mabasi mji mdogo wa CHIMBUYA YA KWANZA,kisha unakodi bodaboda mpaka shuleni au waweza kutembea kwa miguu kwani ni umbali wa 1/2 km tu.
C. MALIPO MBALIMBALI
NA. | AINA YA MALIPO | KIASI (TSH) | WAKATI WA MALIPO |
1. | ADA Ada ya shule kwa mwaka ni Tsh. 1,995,000/= na hulipwa kwa awamu nne. Yaani |
|
|
a) Awamu ya kwanza | 500,000/= | JANUARI: Anaporipoti kwa mara ya kwanza | |
b) Awamu ya pili | 500,000/= | APRIL: Anaporudi toka likizo fupi. | |
c) Awamu ya tatu | 500,000/= | JULAI: Anaporudi toka likizo ndefu. | |
d) Awamu ya nne | 495,000/= | SEPTEMBA: Anaporudi toka likizo fupi. | |
| JUMLA YA ADA KWA MWAKA | 1,995,000/= |
|
2 | SARE Hizi huandaliwa hapa shuleni a) Mashati 2 light blue mikono mifupi (@ 120000 |
24000/= |
JANUARI |
b) Suruali tatu @20,000 - Mbili – dark blue - Moja - nyeusi |
60,000/= |
JANUARI | |
c) Sweta 2 Dark blue @ 12000 | 24000/= | JANUARI | |
| d) T-SHIRT 2 (form six) light blue @ 12000 | 24000/= | JANUARI |
| JUMLA YA SARE | 132,000/= |
|
4 | UMISETA | 1500/= | JANUARI |
D. JINSI YA KUFANYA MALIPO
Malipo yote ya shule hufanyika kupitia Benki kwa utaratibu ufuatao.
NA | AINA YA MALIPO | AKAUNTI NAMBA |
01 | ADA | a) CRDB OSWE BOYS SECONDARY SCHOOL 0150298634500
b) NMB OSWE BOYS SECONDARY SCHOOL 61210029260 |
2 | MICHANGO MINGINE Hii inahusisha malipo mengine yasiyohusisha ada ikiwa ni pamoja na malipo ya: - Malipo ya Sare - Michango ya Umiseta - Fedha za matumizi (Tsh 40,000 kwa kila robo muhula) - Michango ya mitihani kwa kidato cha pili na nne. |
CRDB OSWE BOYS SECONDARY SCHOOL 0150298634501
|
ANGALIZO:
1. Malipo yoyote ya ada hayatarudishwa endapo mwanafunzi atashindwa kuendelea na masomo katika shule hii.
2. Mwanafunzi aliye chaguliwa kujiunga na shule hii haruhusiwi kugawa au kutoa nafasi yake kwa mtu mwingne. Haki ya kuziba pengo ni ya uongozi wa shule tu.
3. Mzazi atatakiwa kuweka fedha kiasi cha Tsh. 100,000/= kuanzia siku anayochukua form hii mwisho tarehe 30/11/2024 kama kielelezo cha kuikubali nafasi hiyo ya mwanao katika shule hii. Aidha mzazi asipofanya hivyo shule itagawa nafasi hiyo kwa mtoto mwingine. Fedha hiyo ni sehemu ya ada ya mwanao.
E. VITU MBALIMBALI AMBAVYO MZAZI/MLEZI ANAPASWA KUVINUNUA NA MWANAFUNZI AJE NAVYO SHULENI.
1. Blanketi moja (1) na shuka mbili za light blue
2. Viatu vyeusi vya kamba, visigino vifupi jozi mbili (2)
3. Socks nyeusi jozi mbili (2).
4. Yeboyebo jozi moja.
5. Jembe moja na mpini wake
6. Dunlop(rain boot) jozi (1)
7. Raba za michezo jozi moja (1)
8. Truck-suit nyeusi mbili zenye mistari mieupe.
9. Bukta ya kulalia rangi nyekundu, mto, foronya (2) za light blue, chandarua rangi ya blue na godoro size 2 ½ x 6.
10. Ndoo moja ya kuogea, kijiko, chombo cha chakula(container) na kikombe.
11. Sanduku la bati ( tranker), kufuli la tranker.
12. Taulo moja, chupi dazani moja, vest mbili (2) rangi nyeupe.
13. Mswaki na dawa ya meno, brush na dawa ya viatu, pia aje na vibanio kwa ajili ya kubania nguozake pindi anapozifua na kuanika.
14. Sabuni za kufulia na za kuogea, mafuta ya kupakaa.
15. Mkanda mweusi usio na matobo matobo wala chuma kikubwa.
16. Tochi moja kwaajili ya tahadhari endapo umeme ukikatika
VIFAA VYA MASOMO AMBAVYO NI LAZIMA MTOTO AFIKE NAVYO SIKU YA KURIPOTI:
1.Kitabu chake cha hisabati (lazima)
2.Faili la kutunza kumbukumbu za mwanafunzi moja (01
3.Kamusi TATU yaani(Kiswahili kwa Kiswahili, kiiingereza kwa Kiswahilina
kiingereza kwa kiingereza)
4. Kalamu za risasi, mfuto, kalamu 10 za wino, rula, mkebe(mathematical set),
daftari aina ya counter book kumi na mbili (12) ukubwa wa 3 au 2 quares,
daftari kubwa la kawaida (1) na daftari ndogo (3) za mwandiko
(mistari midogo na mikubwa).
F. VIFAA VYA KUKABIDHI OFISINI
1. Graph pad mbili (02). (kwa ajili ya shule)
2. Faili la kutunza kumbukumbu za mwanafunzi moja(1) plastic faili ndogo za spring(kwa ajili ya shule)
3. Kitabu cha TIE kimojawapo kati ya masomo yafuatayo (PHYSICS au KISWAHILI au ENGLISH au HISTORYkwa kidato chochote.
4. Rimu 2 za karatasi A4ainaya( TRIDENT ECO GREEN au NO1 ) ZINGATIA IWE 80g/m.kila mwaka .
G. TARATIBU ZA SHULE
1. Ni wajibu wa mwanafunzi kutii na kufuata sheria za shule.
2. Mwanafunzi atakapokuwa anasubiri sare za shule zikiandaliwa atavaa tracksuit,T-shirt na suruali nyeusi
3. Mwanafunzi haruhusiwi kutunza zaidi ya shilingi elfu tatu chumbani, amtumie mhasibu wa shule kutunza fedha zake. Endapo atakutwa na zaidi ya pesa hiyo, pesa hiyo itachukuliwa na kupelekwa benki kama sehemu ya ada yake na hatua za kinidhamu zitachukuliwa juu yake.
4. Ni marufuku mwanafunzi kuja na simu, redio na kamera. Iwapo atakamatwa nayo basi vitu hivyo vitaharibiwa kabisa na mwanafunzi atafukuzwa shule mara moja. Ikiwa kama mwanafunzi anauhitaji wa kupiga simu kwa sababu maalumu,basi mwalimu mlezi atahusika kupiga nakufanya mawasiliano,mwanafunzi haruhusiwi kupiga nakuongea kupitia simu.
5. Mwanafunzi awapo shuleni azingatie sana kusoma. Awapo shuleni lugha ya mawasiliano ni kiingereza tu, haruhusiwi kuongea kiswahili isipokuwa mda wa somo la Kiswahili.
6. Mwanafunzi haruhusiwi kutumia mafuta au kipodozi chochote ambacho kinaweza kubadilisha rangi ya ngozi yake.
7. Mwanafunzi haruhusiwi kunyoa upala,kukali nywele wala kuweka dawa ya aina yoyote.
8. Mwanafunzi haruhusiwi kwenda/kuonekana kwenye kumbi au nyumba za starehe awapo shuleni au nyumbani wakati wa likizo.
9. Shule haitatoa chakula maalum (special diet) kwa mwanafunzi yoyote. Kila mwanafunzi atakula chakula kinacholiwa na watu wote hapa shuleni.
10. Ni marufuku mwanafunzi kwenda nje ya mipaka ya shule, isipokuwa kwa kibali maalum.
11. Ni marufuku kwenda/kuonekana kwenye nyumba ya mfanyakazi yeyote, hata kama nyumba hiyo ipo jirani au katika maeneo ya shule.
12. Endapo mwanafunzi anapita eneo la utawala (smart area) anatakiwa kuonyesha ukakamavu.
13. Nidhamu ni ngao ya shule yetu, kila mwanafunzi anatakiwa kujiheshimu na kuheshimu wenzake bila kujali umri au itikadi zao.
14. Wanafunzi watapata huduma za matibabu ya awali wakiwa shuleni kisha watapelekwa hospital kwavipimo na matibabu zaidi endapo hali zao kiafya hazitatengamaa.
15. Ni marufuku tena mwiko kwa mwanafunzi yeyote kutumia lugha ya matusi, kugombana, uvutaji wa sigara na bangi awapo shuleni hata nyumbani.
16. Marufuku kwa mwanafunzi/ mzazi kuleta chakula shuleni, wanafunzi wote watakula chakula cha shule
17. Visiting day/siku maalumu ya kuwasalimia wanafunzi haitakuwepo. Aidha mzazi anaruhusiwa kuja shuleni kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi, na kukiwepo
ulazima wa kuonana nae atafanya hivyo kwa ruhusa ya mwalimu atakaye husika kwa siku hiyo.
18. Hairuhusiwi mzazi kuingia katika eneo la shule akiwa amevaa mavazi yasiyo ya maadili.
ASANTE,
Gharama ya mafunzo ya pre-form one kwa miezi miwili ni Tsh 200,000/ =
Masomo yataanza tarehe 23/9/2024 mpaka tarehe 20/12/2024
……………………………
SIMCHIMBA MICHAEL, J
MKUU WA SHULE.
...............................................................................................................
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OSWE BOYS SECONDARY SCHOOL P.O. BOX 665 MBOZI – SONGWE EMAIL: osweboys@gmail.com WEBSITE:www.osweschools.ac.tz |
TEL: 0752- 398224 HEAD OF SCHOOL : 0742 - 697782 VICE HEAD OF SCHOOL : 0764 -961755 ACADEMIC |
JINA LA MWANAFUNZI…………………………………TAREHE:..………
JINA LA MZAZI/MLEZI………………………………………………
Mimi mwanafunzi mtajwa hapo juu naahidi kuwa nakubaliana na utaratibu wa shule:
i) Nisipohudhuria vipindi vya kutosha darasani.
ii) Tabia yangu ikiwa haiendani na taratibu za kuboresha taaluma na hatimaye kushindwa kufikisha wastani wa alama za ufaulu wa shule nitarudia darasa.
SAINI YA MWANAFUNZI……………………………………………
A. AHADI YA MZAZI/MLEZI
JINA LA MZAZI/MLEZI ………………………………TAREHE………
JINA LA MWANAFUNZI…………………………………………………
a) Mimi Mzazi/Mlezi wa mtajwa hapo juu naahidi kuwa nitalipa ada kwa wakati kulingana na taratibu za shule. Nisipotekeleza nitakuwa tayari kumpokea mwanafunzi akirudishwa kuja kufuata ada ya shule.
b) Mimi mzazi/mlezi wa mtajwa hapo juu naahidi kuwa nakubaliana na utaratibu wa shule, kwamba mtoto
i) Asipoweza kuhudhuria vipindi vya kutosha darasani
ii) Tabia yake ikiwa haiendani na taratibu za kuboresha taaluma na hatimaye kumfanya mtoto wangu kushindwa kufikia kiwango kinachotakiwa cha ufaulu wa shule atarudia darasa.
…………………………….
SAINI YA MZAZI/MLEZI
NB: Baada ya kujaza fomu hii irudishwe shuleni kwa mkuu wa shule.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OSWE BOYS SECONDARY SCHOOL P.O. BOX 665 MBOZI – SONGWE EMAIL: osweboys@gmail.com WEBSITE:www.osweschools.ac.tz
|
TEL: 0752- 398224 HEAD OF SCHOOL : 0742 - 697782 VICE HEAD OF SCHOOL : 0764 -961755 ACADEMIC |
MEDICAL EXAMINATION FORM
(To be completed by a medical officer in respect of all entrants)
1. Pupil’s full name:………………………………………………………………
2. Eyes examination (eye sight) …………………………………………………
3. Ears examination (Hearing) ……………………………………………………….
4. Chest examination …………………………………………………………………
5. Cardiovascular examination ……………………………………………………….
(a) Pulse …………………………………
(b) Blood pressure ………………………..
(c) Heart sounds ………………………….
6. Gastrointestinal examination ………………………………………..
(a) Spleen ……………………………………..
(b) Liver ……………………………………….
7. Haemoglobin …………………………………………..
8. Blood slide for malaria parasites …………………………………..
9. Stool examination (routine) ………………………………
10. Urine examination (routine) ………………………………
11. Syphilis and other venereal diseases …………………………………….
12. Pregnancy test ……………………………………
13. Any other defects noted in history/examination eg. Epilepsy ………….
14. Is the student fit for a Boarding Secondary School (physically and mentally)? ………………………………………………………………………………
Medical officer’s Name ……………………….……………………….
Signature ………………………………………………………………..
Date ……………………………………………………………………
Official Stamp
(Nakala hii irudishwe shuleni siku ya kuripoti)
(All correspondences should be addressed to the Head of School)